Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano jela miaka 30 kwa unyang’anyi na kujeruhi

9a81b9f872bfe447549e35a73e0dfea1.jpeg Watano jela miaka 30 kwa unyang’anyi na kujeruhi

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, imewahukumu watu watano kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Nzega, Mhere Mwita alisema kutokana na ushahidi usioacha shaka uliotolewa mahakamani hapo mahakama hiyo imeridhia adhabu hiyo.

Mwita alisema kutokana na kukithiri kwa matendo ya uhalifu mahakama inatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho.

Wafungwa hao wapya ni Kulwa Kaseme, Joseph Salumu, Mabula Mmoja, Kiswalo Kulwa na Ngasa Mhumbi.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali, Jenifa Mandago mwaka 2020 watano hao walivamia kwa Simoni Bundala, mkazi wa Kijiji cha Iyombo Wilaya ya Nzega wakiwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga, wakampiga na kumjeruhi na kisha kumuibia kiasi cha Sh 100,000.

Washitakiwa wakijitetea kabla ya kusomewa adhabu baada ya kutiwa hatiani, waliomba kupunguziwa adhabu kutokana na kuwa na familia zinazowakabili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz