Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu wa kudhibiti ufisadi nchini wapatiwa mafunzo

WhatsApp Image 2022 11 15 At 12.jpeg Wataalamu wa kudhibiti ufisadi nchini wapatiwa mafunzo

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa kitengo Cha kudhibiti na kuzuia ufisadi na rushwa kutoka taasisi za umma na binafsi nchini wamepatiwa mafunzo yakusaidia taasisi zao katika kubaini ubadhirifu unaofanywa kwa kutumia mbinu za kiuchunguzi.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyija jijini Arusha wa mapambano dhidi ya ufisadi,Rushwa na ubadhilifu .

Rais wa chama cha wataalamu wa udhibiti,ufisadi,Rushwa na Ubadhirifu (ACFE) Stella Cosmas anasema wamekutana kujadili namna bora ya kuzuia na kupambana na ubadhirifu na masuala ya Rushwa nchini katika taasisi za ndani.

Amesema lengo ni kuisaidia serikali katika kupambana na makosa ya kiufisadi na Rushwa ambapo wameweza kufanya upelelezi mkubwa katika kuhakikisha Tanzania inaondokana na vitendo vya Rushwa.

"Sisi ni wapelelezi wa ndani na ni wataalamu kabisa ambao tuna vyeti ambapo cheti ni Cha Kimataifa na kinapatikana katika nchi 125 na makao makuu ya chama yapo Marekani"Alisema Stella

Aidha amesema katika siku za Mkutano watatoa elimu kwa wataalamu kutosubiri matukio yatokee ndiyo wapeleleze badala yake wapate utaalamu wa kugundua viashiria kabla havijatokea.

Amesema wanaishukuru Serikali kwa kuendelea kupiga vita masuala ya rushwa na wao wanahakikisha wanaiunga mkono kwa kuendelea kupinga vita vitendo hivyo ambavyo vinaikwamisha Serikali ya Rais Samia Suluhu katika maendeleo.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Gladness Msuya afisa viatarishi na ubora kutoka mamlaka ya bandari nchini anasema vyanzo vya rushwa vinabadilika kila mara na hivyo mafunzo kama haya yatasaidia kuendana na teknolojia ili kutumia mbinu mpya na kuweza kuzuia viashiria vya rushwa na ubadhirifu kwa wakati.

"Sisi ndiyo Wataalamu tunaotegemewa kuondoa viashiria hivi vya rushwa na kama tutakuwa na mafunzo mbadala kila mara ni wazi Taasisi hizi zitafika mbali kimaendeleo kwani rushwa, ubadhirifu ni Adui wa ustawi wa maendeleo"Alisema Gladness

Bruno mchopa ni mshiriki kutoka kitengo Cha uchunguzi katika taasisi ya kifedha CRDB Bank anasema zipo teknolojia mbalimbali wanazotumika katika kugundua viashiri mapema na kuzifanyia kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live