Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiojulikana wawaua mama na bintiye

20414 Mauaji+pic TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita, Wakazi wawili wa Kijiji cha Nyakagomba wilayani Geita ambao ni mtu na bintiye, wameuawa kwa kunyongwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana Oktoba 1, 2018.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyangi katika kijiji hicho, Henry Thomas akizungumza na Mwananchi leo amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

Amewataja waliouawa kuwa ni Asteria Kadash (68) na Eliza Thomas (30) ambao waliuawa wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

Kamanda wa Polisi Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema taarifa za tukio hilo atazitoa baadaye.

Chanzo: mwananchi.co.tz