Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasiojulikana waua mmoja kwa mapanga

PANGA Wasiojulikana waua mmoja kwa mapanga

Tue, 5 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MTU mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojuilikana katika Kijiji Cha Nzinza Roho Shengejuu Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis, alimtaja aliyeuawa ni Daudi Deos Mpangala (40), mkazi wa Shengejuu Wilaya ya Wete.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Nzinza Shengejuu majira ya usiku juzi, ambapo walifika watu nyumbani kwake na kumwita ili atoke nje na alipotoka tu walimvamia na kumshambulia kwa mapanga.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi pamoja na kuwasaka waliohusika na tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live