Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya kusafirisha dhahabu wakiri kosa

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza.  Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya jinai namba 1/2019 ya kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 323.6 na fedha taslimu Sh305 milioni wamekiri makosa yao.

Washtakiwa hao ni wafanyabiashara Hassan Sadiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda na Sajid Hassan.

Askari katika shauri hilo ambao wamekana makosa yao ni aliyekuwa mkuu wa operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda, E. 6948 D/CPL. Kasala, F. 1331 PL. Matete, G. 6885 D/C Alex na G. 5080 D/C Maingu.

Wengine ni G. 7244 D/C Timothy, G. 1876 D/C Japhet, H. 4060 D/C David Kadama.

Wakili wa Serikali, Robert Kidando akisoma hati ya mashtaka ameieleza mahakama kwamba washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 10 ya kujihusisha na biashara ya dhahabu bila kibali,  kuomba na kupokea rushwa, utakatishaji wa fedha na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Awali mkurugenzi idara ya makosa ya rushwa, udanganyifu na utakatishaji fedha, Fredrick Manyanda aliiomba mahakama ya ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kubadili hati ya mashtaka na kuipa mahakama hiyo mamlaka ya kusikiliza shauri hilo ambapo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rhodha Ngimilanga amekubaliana na ombi hilo

 



Chanzo: mwananchi.co.tz