Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa meno ya tembo 1,023 waachiwa huru

Meno Ya Tembo Baadhi ya vipande vya meno ya Tembo

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wafanyabiashara watano waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na vipande 1023 vya na meno ya tembo yenye thamani ya Sh7.4 bilioni.

Washtakiwa hao wameachiwa leo Jumatatu Machi 21, 2022 baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Uamuzi wa kuwaachia huru washtakiwa hao, umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Walioachiwa huru katika kesi hiyo, PI namba 19/2015 ni Mohamed Musa, Mohamed Haji maarufu kama Udole, Juma Makame, Mohamed Mashaka na Omary Ally, wote wakazi wa Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live