Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa kwa utakatishaji wa milioni 168/-

7648507e40d279732a3f629f3979611d Washtakiwa kwa utakatishaji wa milioni 168/-

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa ya wizi na utakatishaji wa fedha zaidi ya Sh milioni 168.

Washtakiwa hao Fred Manjiu mkazi wa Kimara Temboni na Arbogast Christian mkazi wa Mkuranga wamefikishwa mahakamani hapo kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu huku upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Martenus Marandu akisaidiwa na Wakili wa Serikali Kija Luzungana.

Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo aina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo huku wakili Marandu akidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba siku nyingine ya kutajwa shauri hilo.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Desemba 24, 2020 na washtakiwa walipelekwa mahabusu kwa kuwa moja ya mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Chanzo: habarileo.co.tz