Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa kesi ya dhahabu wakacha kifungo, walipa faini

49416 WASHTAKIWA+PIC

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya jinai namba 1/2019 ya kusafirisha shehena ya dhahabu kilo 319 na fedha taslimu Sh305 milioni waliohukumiwa adhabu ya vifungo jela kati ya miaka mitano hadi 15 au kulipa faini kati ya ya Sh5 milioni hadi Sh100 milioni wameachiwa huru baada ya kulipa faini ya jumla ya Sh529.8 milioni.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, Rhodha Ngimilanga aliyetoa hukumu hiyo amethibitisha kuwa washtakiwa wote ambao ni wafanyabiashara Hassan Sadiq, Emmanuel Mtemi, Kisabo Nkinda na Sajid Hassan wamelipa faini na kuachiwa huru leo Ijumaa Machi 29, 2019.

Washtakiwa hao walihukumiwa juzi Jumatano Machi 27, 2019 baada ya kukiri mashtaka ya kutoa na kupokea rushwa, kujihusisha na vitendo vya rushwa na kutakatisha fedha.

Mmoja wa mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Anthony Nasimile amesema wateja wake sasa wako huru baada ya kukamilisha malipo ya faini na taratibu zote za kisheria.

Pamoja na hukumu ya kifungo kwa muda tofauti na faini kulingana na kosa Mahakama pia imetaifisha kilo 319 za dhahabu zenye thamani ya Sh27.018 bilioni, fedha taslimu Sh305 milioni, magari mawili, kilo sita za madini ya vito, mashine ya kupima ubora na mizani ya kupimia madini.

Wakati wenzao wakikiri makosa, kulipa faini na kutoka magereza, washtakiwa wengine wanane ambao wote walikuwa askari polisi akiwemo aliyekuwa mkuu wa operesheni mkoa wa Mwanza, Morice Okinda wamekana mashtaka na kesi yao inatarajiwa kuendelea kusikilizwa Aprili 10, 2019 baada ya upelelezi kukamilika.

Wengine ambao kesi dhidi yao inaendelea ni E. 6948 D/CPL. Kasala, F. 1331 PL. Matete, G. 6885 D/C Alex, G. 5080 D/C Maingu, G. 7244 D/C Timothy, G. 1876 D/C Japhet na H. 4060 D/C David Kadama.

Soma zaidi>> Utata wagubika kesi shehena ya dhahabu

  >>Kesi ya dhahabu ya Sh27 bilioni yapigwa kalenda

>>Mpakistan aliyefungwa kesi ya dhahabu kufukuzwa Tanzania

>>Washtakiwa wanne kati ya 12 wa kesi ya kusafirisha dhahabu wakiri kosa

>>Washtakiwa kesi ya dhahabu wahukumiwa



Chanzo: mwananchi.co.tz