Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa kesi ya almasi waomba watumie fedha za kwenye akaunti zao

58860 Pic+washtakiwa

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mkurugenzi uthaminishaji almasi,  Archard Kalugendo na mthamini madini ya almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu washtakiwa waruhusiwe kutumia fedha zao zilizoko kwenye akaunti.

Wakili wa Serikali Nehemia Nkoko amedai leo Mei 21, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaid baada ya wakili wa Serikali Wankyo Saimoni kueleza kuwa wako hatua za mwisho kukamilisha upelelezi na jalada limerudishwa polisi kwa ajili ya taratibu za upelelezi zaidi.

Upande wa utetezi katika hoja yake ulidai kuwa washtakiwa wanaendelea kulipwa mshahara, wote wana familia na wanategemea mshahara huo hivyo wanaomba wapewe uwezo wa kutumia fedha zao ili ziweze kuhudumia familia zao.

Hakimu Shahidi aliushauri upande wa utetezi kuwasilisha maombi hayo kwa njia ya maandishi ili yaweze kufanyiwa kazi na mamlaka zinazohusika.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 3 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na kesi ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana.

Kalugendo na Rweyemamu, ambao ni watumishi wa Wizara ya Madini, kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo,  Septemba 15, 2017, wakikabiliwa na  shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4 bilioni.

Pia Soma

Katika hati ya mashtaka, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na mkoani Shinyanga.

Kwa pamoja wakiwa wathaminishaji almasi wa Serikali na waajiriwa wa Wizara ya  Nishati na Madini, waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na Sh2.4bilion.

Chanzo: mwananchi.co.tz