Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washtakiwa kesi ya Luck Vincent wakutwa na hatia, wahukumiwa

61980 Pic+luck

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na makosa yote matano Innocent Mushi ambaye ni mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vincent na Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Longino Vicent.

Hukumu ya kesi hiyo inayowakabili Mushi na Vicent inatoka na ajali ya gari iliyotokea Mei 6, 2017 na kuangamiza wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja inasomwa leo Jumatatu Juni 10, 2019 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama, Niku Mwakatobe.

Hakimu Mwakatobe amesema mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mushi atatakiwa kulipa faini ya Sh1.5 milioni akishindwa atatumikia kifungo cha miaka minne na miezi sita gerezani na mshitakiwa wa pili, Vicent kulipa faini Sh500,000 akishindwa atatumikia jela mwaka mmoja.

Ajali hiyo, ilitokea Mei 6, 2017, katika eneo la Rhotia wakati, wanafunzi wa shule hiyo, wakitoka Arusha majira ya saa 12 asubuhi kwenda wilayani Karatu, katika mitihani ya ujirani mwema katika Shule ya Tumaini Academy.

Makosa hayo matano ambayo Hakimu Mwakatobe amewakuta na makosa hayo matano ni; kuvunja sheria za usalama barabarani ikiwemo kuendesha gari za abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, gari lililosababisha ajali kutokuwa na bima, kushindwa kuingia mkataba baina ya dereva na mwajiri na kosa la kuzidisha abiria 13 katika gari lililopata ajali ambalo linamkabili mwalimu mkuu msaidizi.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz