Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washikiliwa na polisi kumuua baba yao, kumkata sehemu za siri

Rpc Kuzagaa.webp Washikiliwa na polisi kumuua baba yao, kumkata sehemu za siri

Wed, 13 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

???????JESHI la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu 4, watatu wakiwa ni familia moja kwa tuhuma za kumuuwa kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni baba yao mzazi Lumba Nhalima (57) Kisha kumkata sehemu zake za siri.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika Kijiji cha Kasekese wilayani Tanganyika mkoani Katavi, wakati marehemu akitoka kunywa pombe na kuelekea nyumbani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi, Benjamin Kuzaga, amesema siku ya tukio watuhumiwa walimnywesha pombe nyingi marehemu ili ashindwe kujitambua.

Kuzaga amesema marehemu akiwa njiani kurudi nyumbani alikutana na watuhumiwa hao ambao ni Sali Lumba ( 32), Jonas Lumba (28), Paulo Lumba (19) na Thomas Malongo (54) ambaye alikuwa anakunywa naye pombe.

Aidha, Kuzaga amesema baada ya uchunguzi walibaini kabla ya kifo chake marehemu alikuwa akilalamika kuwa watoto wake wakubwa wanne ambao niwa mke mkubwa aitwaye Wande Mabuki (46) kuwa wanataka kumuuwa ili warithi mali zake.

Kuzaga amesema chanzo cha kifo chake kinahusishwa na imani za kishirikina pamoja na tamaa za kurithi mali, hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya msako mkali kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

Watuhumiwa hao wamekili kuhusika kupanga njama na kufanikisha mauwaji hayo. Hata hivyo jeshi hilo linatoa rai kwa wananchi wa Mkoa huo kuachana na dhana potofu za kujipatia kipato kwa njia ambazo si halali ikiwemo njia ya imani za kishirikina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live