Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapandishwa kizimbani kwa kuisababishia Tanesco hasara ya Sh 930 milioni

11799 Tanesco+pic TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Walinzi wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka wawili, likiwamo la kuisababishia hasara ya Sh 930milioni, Shirika la Umeme nchini (Tanesco) baada ya kukata nyanya za Umeme.

Washtakiwa hao katika kesi ya Uhujumu uchumi namba 53 ya mwaka 2018 ni Rafael  Kisaucha(24)mkazi wa Gongolamboto na Athuman Shekiufya(26)mkazi wa Ubungo Kibangu.

Pia washtakiwa hao, wanadaiwa kukata kebo zenye nyaya za umeme mali ya Tanesco, katika eneo la  Ubungo Maziwa.

Wakili wa Serikali Grace Mpatili akisaidiana na Elizabert Mkunde alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega, kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya Uhujumu Uchumi.

Mpatili alidai kuwa katika shtaka la kwanza, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa, Julai 3 2018 eneo la Ubungo Maziwa Dar es Salaam, walifanya uharibifu kwa kukata kebo za umeme, mali ya Tanesco.

Katika shtaka la pili inadaiwa siku na eneo hilo, washtakiwa hao waliisababishia hasara Serikali ya Sh 930milioni kutokana na kukata kebo za nyaya za umeme na hali iliyosababisha kukata Umeme.

Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa hawakurusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kutokana na mahakama hiyo kuwa  haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hadi wapate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP).

Hakimu Mtega aliahirisha kesi hiyo hadi, Agosti 2, mwaka huu itakapotajwa na   washitakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

mwisho

 

Chanzo: mwananchi.co.tz