Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wanaswa na nyara za Serikali Liwale

Meno Pic Data Wanne wanaswa na nyara za Serikali Liwale

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Watu wanne wanashikiriwa na Jeshi la Polisi mkoani Lindi baada ya kukutwa na meno sita ya tembo na vipande 30.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Novemba 16, 2021 na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kitinkwi amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika Kijiji cha Mbonde tarafa ya Liwale katika nyumba ya kulala wageni wakiwa na meno ya tembo mazima sita na vipande 30.

Amesema watuhumiwa walihifadhi meno hayo ambayo yana uzito wa kilo 99 kwenye mifuko.

Amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na operesheni ya polisi ya kusaka wahalifu.

Pia, Kamanda Kitinkwi ametoa wito kwa watu wanaomiliki silaha kinyume na sharia kusalimisha silaha hizo kwa hiyari.

"Nawaomba watu wote kuacha kufanya vitendo vya kihalifu badala yake wajikite katika shughuli halali za kujipatia kipato" amesema kamanda Kitinkwi.

Chanzo: mwananchidigital