Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wanaswa na meno ya tembo

C1d5a6004e14b02be583475c8b80bc65.jpeg Wanne wanaswa na meno ya tembo

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WATUHUMIWA watatu wa ujangili wamenaswa wakiwa na meno 4 ya tembo yenye uzito wa kilogramu 21.2.

Meni hayo inadaiwa yalikuwa yakisafirishwa kutoka Inyonga katika wilaya ya Mlele Mkoani Katavi kuja Mkoani Tabora.

Hayo yamebainishwa jana na Kamanda wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) Kanda ya Magharibi, Bigilimungu Kagoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake mjini hapa.

Alisema watuhumiwa hao waliokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki aina ya Sun LG yenye namba za usajili T 616 DBE Watu hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora na kesi yao inaendelea.

Kamanda Kagoma aliongeza kuwa pia walifanikiwa kunasa majangaili 3 wakiwa na silaha aina ya Riffle 458 yenye nambari 7152603774 ikiwa na risasi 3 na gobole 1 katika Msitu wa Hifadhi wa Nyahua ulioko wilayani Sikonge . Katika doria kwenye Msitu wa Hifadhi wa Kigwa/Lubuga wilayani Uyui jangili mmoja aliyekuwa akiwinda wanyamapori ndani ya hifadhi hiyo alitupa silaha yake aina ya Riffle.458 yenye namba 735250548 na kutokomea kusikojulikana baada ya kuwaona askari hao.Aliongeza kuwa silaha nyingine 2 zinazosadikika kutumika katika matukio ya ujangili zilisalimishwa katika ofisi ya serikali ya kijiji cha Goweko wilayani Uyui Mkoani Tabora, wahusika walijisalimisha na kuomba msamaha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz