Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wakamatwa kwa kutapeli Mil. 10 Zanzibar

NANE KWA UTAPELI Wanne wakamatwa kwa kutapeli Mil. 10 Zanzibar

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne ambao wanafanya vitendo vya kitapeli katika maeneo yanayotoa huduma za kifedha Jijini Zanzibar

Akitoaa taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Richard Mchomvu amesema mnamo tarehe 19 Juni, 2023 majira ya saa 4 asubuhi nje ya benki ya CRDB Tawi la Zanzibar iliyopo Mchenzani Mall, watuhumiwa hao walimtapeli mwananchi fedha ya shilingi Milioni kumi (10,000,000)

Kamamda Mchomvu amesema baada ya uchunguzi kupitia CCTV Camera Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuitambua gari iliyotumika katika utapeli huo yenye namba za usajili Z 971 HZ aina ya Alphad rangi nyeupe ambayo iliyokua ikiendeshwa na dereva aitwae masoud Ali Suleiman '48' Mshirazi wa fuoni

watuhumiwa wengine watatu ni Yakoub Joseph Yakoub '28' msukuma wa Kinondoni, Michael masunga Gonald '50' msukuma wa Kinondoni na mwengine ni Yerem badru athumani '48' Mhaya wa Temeke Dar-es-salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live