Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wakakamatwa tuhuma za mauaji ya ofisa ustawi Mbeya

Kujinyonga Data Wanne wakakamatwa tuhuma za mauaji ya ofisa ustawi Mbeya

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanne akiwamo aliyekuwa mume wa Gloria Kabila anayedaiwa kunyongwa hadi kufa siku mbili zilizopita jijini hapa.

 Gloria ambaye aliuawa siku mbili zilizopita alikuwa ofisa Ustawi wa Jamii katika kituo cha mahabusu ya watoto kilichopo mtaa wa Kabwe Kata ya Iyela jijini Mbeya.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 6, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC), Urlich Matei amesema kutokana na mazingira ya kifo hicho tayari wamemshikilia aliyekuwa mume wa marehemu ambaye walizaa wote watoto watatu kabla ya kutengana.

Amesema kuwa wamemkamata baada ya kufuatilia mawasiliano kwenye kwenye simu yake.

"Kabla ya kifo chake alienda kazini akawakuta wafanyakazi wenzake akawaaga anaenda kunywa mtori kwenye mgahawa wa Chaga Night uliopo karibu na kituo cha kazi baadaye alienda nyumbani na hakurudi tena kazini hadi alipokutwa amenyongwa" amesema Matei na kuongeza

"Baada ya vipimo vya daktari jana Jumamosi vilibaini kuwa marehemu alinyongwa, hivyo tunaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo zaidi" amesema Kamanda huyo.

Advertisement

Chanzo: www.mwananchi.co.tz