Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Wed, 18 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi.  Mahakama Kuu Kanda imewahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia kinyume cha kifungu cha sheria 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyorekebishwa 2002.

Jaji wa Mahakama hiyo Dk Adam Mambi akisoma hukumu hiyo leo Jumanne Septemba 17, 2019 amesema Mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na baada ya kujihoji kuhusu lengo la washitakiwa.

Amewataja washitakiwa hao kuwa ni Nathan Elias (31) mkazi wa Mwaka Tunduma, Moses Kasitu (26) mkazi wa Kilimahewa Tunduma na Elias Mzumbwe(23) mkazi wa Ihanda Mbozi.

Amesema wote walishiriki kumuua Vasco Njowela kwa kumpiga risasi kiunoni na kumnyang'anya mfuko uliokuwa na fedha za mauzo ya dukani kiadi cha Sh1 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz