Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne mikononi mwa polisi kwa kutaka kumuozesha mwanafunzi

60810 Pic+polisi

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Jeshi la polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu wanne kwa madai ya kutaka kumuozesha mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lwamgasa.

Wanaoshikiliwa ni baba wa binti huyo, Kueyema Malongo (78) ambaye alipewa ng’ombe sita na mbuzi wawili kama sehemu ya mahari ili mwanaye aolewe.

Wengine ni washenga, Ishel Makeregese (50), Mengi Edward (31) na baba wa muoaji, Elias Charles.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,  Mponjoli Mwabulambo amesema wanaendelea kumsaka aliyekuwa akitaka kumuoa mwanafunzi huyo kwa maelezo kuwa alikimbia baada ya polisi kufika katika sherehe ya kutoa mahari iliyofanyika nyumbani kwa mwanaume huyo.

Amesema taarifa za binti huyo kuozeshwa zilitolewa na walimu wake waliodai kuwa aliwaeleza iwapo hataolewa atajiua jambo lililowashtua na kuamua kutoa taarifa polisi.

Chanzo: mwananchi.co.tz