Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne mikononi mwa Polisi kwa ujangili

19224857 905 Wanne mikononi mwa Polisi kwa ujangili

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: Dar24

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera, linawashikilia watu wanne waliojihusisha na ujangili wa nyara za Serikali katika Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa na Rumanyika Karagwe.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema watuhumiwa wote walikamatwa Februari 13 mwaka huu katika Kijiji cha Muungano, Kata Lusahunga Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa na nyara hizo kuwa ni Raphael Lugaira (44), Fikiri Lugaira  (43), Majaliwa Charles (42) na Warwa Rupily (45), wote wakazi wa Wilaya ya Biharamulo.

Kwa mujibu wa Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi, Hifadhi ya Taifa ya Ibanda Kyerwa, Frederick Mofulu alisema walipata taarifa za uwepo wa wahalifu wanaoua wanyama ambapo walishirikisha Jeshi la Polisi na kuwakamata watuhumiwa hao.

Amezitaja nyara zilizokamatwa kuwa ni meno mawili ya tembo, ngozi ya fisi, kichwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati, mkia wa nyati na ngozi ya swala na kwamba watuhumiwa hao walikamatwa na silaha mbili aina ya gobole pamoja na risasi tatu za kienyeji aina ya gololi.

Chanzo: Dar24