Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya kukata na mapanga

PANGA Ed Wanne mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya kukata na mapanga

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya watuhumiwa wanne wa mtandao wa mauaji kwa kutumia njia ya ukataji mapanga wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga baada ya kufanyika kwa Msako katika Mkoa huo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP-Leonard Nyandahu amesema watuhumiwa hao wamekatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

“Tumefanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wanne wanaojihusisha na ukataji wa mapanga, mmoja akiwa kama mdhamini, anawapa pesa wanafanya uhalifu huo.

"Katika mahojiano wote wamekiri kufanya matukio hayo katika maeneo mbalimbali. Kwa sasa jeshi la polisi linakamilisha taratibu ili waweze kufikishwa mahakamani," amesema Kamanda Nyandahu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live