Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne mbaroi wizi vifaa vya reli ya kisasa

MBARONI.jpeg Wanne mbaroi wizi vifaa vya reli ya kisasa

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wamekamatwa wakiwa na vipande 390 vya nondo za ukubwa wa milimita 16 zilizokuwa awali zimejengea uzio kuzuia kukatiza wanyama waharibifu ikiwemo tembo katika reli ya kisasa ya mwendo Kasi.

Aidha mkoani Dodoma nako amekamatwa mtu mmoja Elia Elias, 24, maeneo ya Makulu akiharibu miundombinu hiyo ya Reli kwa kubomoa nguzo nane za uzio wa SGR kwa kuzivunja kwa kutumia nyundo kubwa na kuchukua nondo zilizomo ndani yake kwaajili ya kwenda kuziuza kama vyuma chakavu.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, Kamishna msaidizi wa polisi (ACP) Sebastian Mbuta, amefika eneo la tukio na kujionea uharibifu huo sambamba na kufika kituo cha Polisi Ngerengere kushuhudia nondo zilizokamatwa.

ACP Mbuta amebainisha katika tukio la Ngerengere, tayari wamewatia mbaroni Florah Mbago, 39, mkazi wa Kiburumo Ngerengere na Juma Kijiti KItu, 66, mkazi wa mgudeni Ngerengere waliokutwa na vipande 17 vya nondo za ukubwa wa milimita 16, mali ya kampuni ya nchini Afrika Kusini ya Rubis, waliopewa kandarasi ya kujenga kilometa 16 za uzio huo wa kuzuia wanyamapori kuvuka upande mmoja kwenda mwingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live