Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne kortini kwa kukutwa na nyama ya kiboko

60384 Pic+kiboko

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

T: Wanne kortini kwa kukutwa na  nyama ya kibok

Dar es Salaam. Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kukutwa na kilo 200 ya nyama ya kiboko yenye thamani ya Sh3.44milioni.

Washtakiwa hao ni Ayoub Kayanda, Jumanne Sia, Said Lwambo na Ally Nongu.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumatano Mei 29, 2019 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi, Augustine Rwizile, wakili wa Serikali, Sada Mohamed  amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 44 ya mwaka 2019.

Amedai katika kosa la kwanza la kukutwa na nyara za serikali kwa pamoja wanadaiwa Mei 9, 2019 wakiwa Nzasa Wilaya ya Temeke walikutwa na kilo hizo  huku wakiwa hawana kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.

Katika shtaka la pili la kujihusisha na nyara za Serikali wanadaiwa kwa pamoja kati ya Mei 7 na 9, 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani walikubali kusafirisha kilo 200 za nyama ya kiboko.

Pia Soma

Saada amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine.

Hakimu Rwizile amesema washtakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote baada ya kuibuka hoja kama mahakama hiyo inapaswa kusikiliza kesi hiyo ama la.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 31, 2019 na washtakiwa kurudishwa rumande.

Chanzo: mwananchi.co.tz