Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne kizimbani kwa kuiba Sh 480m za msikiti

Hukumu Pc Data Wanne kizimbani kwa kuiba Sh 480m za msikiti

Tue, 4 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shata la wizi wa Sh480, 509, 088 ni fedha za msikiti wa Shree Sanatan Dharma uliopo jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao ni Kshary Motichand (22) Mkazi wa Kisutu, Vasant Solanki (73) mkazi wa Jamatin, Ramesh Shash (62) Mkazi wa Zanaki na Shailesh Chauda (48) Mkazi wa Ilala.

Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud amewasomea hati ya mashtaka na kudai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili la wizi na kula njama.

Aboud amedai kuwa kati ya Januari na Novemba 2016 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam wote kwa pamoja walikula njama kwa nia ya kutenda kosa.

Katika shtaka la pili tarehe isiyojulikana na miezi hiyo hiyo wakiwa maeneo hayo wote kwa pamoja waliiba kiasi cha Sh 480,509,088 mali ya msikiti wa Shree Sanatan Dharma huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria

"Upelelezi bado haujakamilka naiomba mahakama yako ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amesema wakili Aboud.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya alisema dhamana ipo wazi kila mshtakiwa awe na wadhamini wawili kati ya hao mmoja awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh60, 000,000.

Hata hivyo mshtakiwa Motichand amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana na washtakiwa watatu wametoka nje kwa dhamana.

Isaya ameahirisha shauri hilo hadi Januari 14, 2022 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live