Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne akiwamo askari polisi mbaroni tuhuma za mauaji

Matei1 Wanne akiwamo askari polisi mbaroni tuhuma za mauaji

Wed, 24 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

POLISI mkoani hapa inawashikilia watuhumiwa wanne akiwamo askari polisi kwa tuhuma za kumuua dereva bodaboda Erasto Mwalwego (29), mkazi wa Nzovwe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, miongoni mwa watuhumiwa hao ni askari wa polisi John Kaijage (34), mkazi wa Isyesye.

Aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Fotunatus Kagande (23), Petson Daniel (22) na Jastini Kagande (27), ambaye ni mwanafunzi.

Alisema tukio hilo la mauaji lilifanyika Juni 20, saa tatu usiku katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Iwambi baada ya watuhumiwa kumshambulia Mwalwego kwa kitu butu.

Alisema Malwego alipelekwa Hospitali ya Rufani Kanda ya Mbeya kwa matibabu na Juni 21 alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

“Jeshi la Polisi tunaendelea na upelelezi kubaini chanzo cha mauaji haya ya kijana Erasto Mwalwego dereva bodaboda na baada ya kukamilika shauri litapelekwa mahakamani ili watuhumiwa kujibu tuhuma za kuhusika na tukio hilo,” alisema Matei.

Katika tukio lingine polisi imemkamata Bahati Ndinagwe, mkazi wa Kijiji cha Kilwa, Kata ya Kajunjumele, wilayani Kyela kwa tuhuma za kughushi nyaraka za serikali ambayo ni barua inayoonyesha kuwa imetoka Ofisi ya Usalama wa Taifa makao makuu kwenda kwa mtuhumiwa huyo ikimjulisha kuwa ameteuliwa kujiunga na Idara hiyo ya Usalama wa Taifa.

Matei alisema barua hiyo ilieleza kuwa lengo lilikuwa ni kupata ajira huku akihitaji kuchapa barua hiyo kwa namna inayofanana na barua za Idara za Uhamiaji ili apate ajira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live