Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume na wavulana washirikishe kutokomeza ukeketaji

Wanaume Na Wavulana Washirikishe Kutokomeza Ukeketaji Wanaume na wavulana washirikishe kutokomeza ukeketaji

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ferbuari 6 ni siku ya kupinga Ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake duniani, Jamii imeaswa kuwashirikisha Wanaume na Wavulana katika kupinga mila na desturi zenye madhara ili kutokomeza ukeketaji

Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Ahadi Ijumaa Msangi aliyemwakilisha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Arusha, katika Shule ya Msingi mkono, kwamba zipo mila na desturi zinazohamasisha ukeketaji kwani mwanamke ambaye hajakeketwa kwa baadhi ya jamii ni vigumu kuolewa na hata akiolewa ana;lazimishwa kukeketwa ili aendane na mil ana desturi za eneo husika.

Amesisitiza kuwa wanaume na wavulana wanaweza kujipima na kukataa ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike na kuona ni kwa namna gani wanaweza kusaidia kupunguza na kukabiliana na vitendo hivyo na kutatua changamoto zinazojitokeza katika mapambano hayo na kubuni mbinu na mikakati mipya

Aidha Msangi alisema kuwa ukeketaji bado ni tatizo na hilo linatokana na baadhi ya jamii kuendeleza kukumbatia mil ana desturi zenyenye madhara na kuwadhalilisha watoto wa kike, ambapo madhara yake ni pamoja na maambukizi ya VVU/UKIMWI,na kusababisha matatizo wakati wa kijifungua.

’’Wakati wa kujifungua watoto wanashindwa kuhudhuria shuleni kwenye vipindi kwa muda mrefu na hivyo kuzorotesha maendeleo ya kielimu’’ Alisema.

Sambamba na hayo alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na jitihada za kukabiliana na vitendo hivyo kupitia mpango mkakati iliyowekwa ikiwemo kutunga na kufanya marekebisho ya sheria na sera mbalimbali za nchi.

Aidha risala ya watoto wa kike kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kupinga ukeketaji ,waliweza kuishukuru serikali katika kutetea haki na maendeleo ya mtoto haswa katika Nyanja za Afya na Elimu ,kuanzisha vyombo mbalimbali na kushirikiana na Mashirika ya Taasisi mbalimbali katika kutetea haki na maslahi yam toto.

Aidha risala iyo iliendelea kusema kuwa pamoja na jitihada zote za serikali bado hali yam toto haijafikia kiwango cha kuridhisha hivyo ili kufikaia kiwango hicho cha lirudhisha wao watoto wakike wamekuja namapendekezo yao .

Ikiwemo kupendekeza maboresho ya sheria ya ukeketaji ijumuishe adhabu kali kifungo na iwahusishe wazwee wa kimila wanaosimamia vitendo hivyo viovu,serikali na kupitisha sheria ya kuzuia ukeketaji nchini

Sambamba na hayo walipendekeza viongozi wa kada mbalimbali nchini na madhehebu ya dini kujitokeza waziwazi na kuunga jitihada zinazoendelea za kutokomeza ukeketaji nchini ,sambamba na Serikali kupitia wizara za kisekta kutenga bajeti ya kupanga utekelezaji wa mapango wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji wa mwaka 2021-2024.

Aidha wameiomba SERIKALI,wadau wote wa maendeleo Viongozi wa kimila ,Mahakama na Taasisi za ulinzi na usalama kuwa wanaposema utetezi wa haki na ulinzi wa mtoto wawe wanamaanisha na usiwe kama wimbo,mikakati katika kuyaadhimisha maadhimisho bali wawe wanapanga mipango ,itekelezwe juu ya matukio yake.

Aidha maadhimisho hayo ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji kwa mwaka 2023 Wanaume na wavulana tushirikiane kupinga mila na desturi zenye madhara ili kutokomeza ukeketaji.ikiwa inalenga kuhamasisha jamii kukomesha vitendo vya ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live