Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaotuhumiwa kuiba gari la Ngawaiya, waachiwa, wakamatwa tena

24588 Pic+mahakama TanzaniaWeb

Wed, 31 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imewapandisha Kizimbani mkazi wa Morogoro, Rosemary Samweli na Mkazi wa Chanika, Dar es Salaam, Ibrahim Salum (25) kwa kosa la kuiba gari aina ya Noah yenye thamani ya Sh16 milioni ambayo ni mali ya aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini(CCM),Thomas Ngawaiya.

Awali washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Juni 4 mwaka huu lakini leo hii mahakama hiyo iliwafutia kesi hiyo na mahakama hiyo iliamuru iwakamate tena na kuwapeleka kituo cha Kidogo cha polisi cha Urafiki.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo na Hakimu Caroline Kiliwa baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Kesi hiyo namba 243/2018 ilitajwa jana mbele ya hakimu huyo huyo na wakili wa Serikali Nancy Mushumbuzi alidai kuwa upande wa mashtaka bado hawajapata taarifa zozote kwa kuwa jalada lipo polisi kwa ajili ya taratibu za upelelelzi.

Hakimu Kiliwa alisema alishatoa nafasi ya mwisho kwa upande wa mashtaka wafuatilie jalada hilo ili waweze kutambua upelelezi umefikia wapi lakini walishindwa kutekeleza agizo hilo.

" Nilishatoa agizo kwa upande wa mashtaka wafuatilie jalada ili wajue upelelezi umefikia hatua gani kwa kuwa hakuna kilichofanyika hivyo leo hii tumewafutia mashtaka kwa kuwa upelelezi haujakamilka,"alisema Kiliwa.

Kesi hiyo iliposomwa Septemba 29 mwaka huu mbele ya hakimu Kiliwa wakili wa Serikali Nancy alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa ila upande wa mashtaka hawakupata maelezo kuhusu jalada la kesi hiyo hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Kiliwa alisema hii ni mara ya mwisho, hivyo aliwataka upande wa mashtaka kufuatilia jalada hilo watambue upelelezi umefikia hatua gani la sivyo atatoa uamuzi wa kuondoa shauri hilo.

Desemba 15 mwaka 2017 eneo la Manzese jiji Dar es Salaam mkazi wa Kilosa, Adamu Ngala (35) na mkazi wa Chanika Ibrahim Magongo (25) waliiba gari aina ya Noah yenye namba T 261DFG  yenye thamani ya Sh16 milioni ambayo ni mali ya Ngawaiya.

Chanzo: mwananchi.co.tz