Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaokabiliwa na mashtaka 601 kupelekwa mahakama ya mafisadi

38316 TRA+PIC Wanaokabiliwa na mashtaka 601 kupelekwa mahakama ya mafisadi

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili mfanyabiashara Mohamed Mustafa Yusufali na Arifal Paliwala umesema unaandaa taratibu za kufungua mashtaka katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ufisadi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 601 likiwemo la kula njama, kughushi nyaraka mbalimbali, kuwasilisha mahesabu ya uongo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kukwepa kodi, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh14.9 bilioni.

Leo Alhamisi Januari 24, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwizile amedai upelelezi umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuandaa taarifa ya kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ufisadi.

Hakimu Rwizile baada ya kusikiliza maelezo hayo ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, 2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Katika shtaka la kwanza washtakiwa wanadaiwa kati ya Januari 2008 na Januari, 2016 jijini Dar es Salaam wakiwa na watu wengine ambao hawapo mahakamani walisambaza vifaa vya ujenzi vikiwa na ongezeko la thamani huku wakijua ni kosa.

Katika shtaka lingine washtakiwa hao walitakatisha fedha kati ya Desemba 2009 na Novemba 2011 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Shtaka lingine kati ya Januari 2008 na Januari 2016 katika maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam washtakiwa hao kwa makusudi na wakijua ni kosa waliwasilisha nyaraka za uongo kwa kamishna wa TRA na kuisababishia Serikali hasara ya Sh14 bilioni huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz