Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kutaka kuchoma moto nyumba ya Katambi wakamatwa

Buses Ed Wanaodaiwa kutaka kuchoma moto nyumba ya Katambi wakamatwa

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Polisi Mkoani Shinyanga imewakamata watu tisa kwa tuhuma za kutaka kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi kupitia CCM.

Miongoni mwa watuhumiwa ni aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CHADEMA, Salome Makamba, ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana.

Watuhumiwa wengine ni wanaume nane wanaoendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika, watawafikisha Mahakamani.

Watuhumiwa waliposhawasha moto, Katambi na wenzake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje na wakaona moto ukiwaka huku pembeni yake kukiwa na dumu lenye mafuta ya petroli ndipo wakanza kuzima moto huo.

MBUNGE MTEULE “NIMENYOOKA SITAANGALIA MTU, NAJUA NITAPATA MAADUI”

Chanzo: millardayo.com