Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kupora vinywaji kwa silaha warudishwa rumande

Pombe Ed Pombe

Fri, 9 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Watuhumiwa hao ni Severin Mkumi, Erick Rwehumbizi, Engeleberth Chiwalo, Salma Mohamed pamoja na Veronica Ismail.

Akiwasomea shtaka lao leo Julai 8, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Luambano, wakili wa Serikali, Yusuph Abood amedai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 112/2021 na wamedaiwa kutenda kosa hilo Juni 26, 2021 eneo la Mikocheni B wilayani Kinondoni.

Amesema, siku ya tukio washtakiwa kwa pamoja waliiba katoni 717 za Hennessy zenye thamani shilingi 408, 650,226 ambayo ilikuwa mali ya kampuni ya MMI Tanzania PVT Ltd.

"Washtakiwa hawa kabla na baada ya kufanya wizi huo, wanadaiwa kumtishia Philipo Jeremiah kwa bastola ili waweze kujipatia vinywaji hivyo bila kikwazo," amedai Abood.

Hakimu Mwandamizi Luambano amesema kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha linalowakabili washtakiwa halina dhamana kwa mujibu wa sheria na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 22, 2021 huku washtakiwa wakirudishwa rumande, kwa kuwa washtakiwa hawakutaliwa kujibu chochote baada ya kusomewa shtaka lao.

Chanzo: ippmedia.com