Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kumwekea mwanamke dawa kupumbaza kusomewa PH Juni 29

Hukumu Pc Data Wanaodaiwa kumwekea mwanamke dawa kupumbaza kusomewa PH Juni 29

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Juni 29, 2022 kumsomea hoja za awali (PH) mfanyabiashara Borgias Kwitega na wenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kubaka na kumwekea vidonge vya kupumbaza kwenye kinywaji mwanamke mwenye umri wa miaka 30 na kisha kumuibia vitu vyenye thamani ya Sh3.3 milion.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace Mwanga ameieleza Mahakama hiyo leo Juni 13, 2022, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira, baada ya upelelezi wa shauri hilo la jinai namba 64/2022 kukamilika.

Mwanga baada ya kueleza hayo, Hakimu Rugemalira ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 29, 2022 itakaitwa kwa washtakiwa kusomewa hoja za awali.

Mbali na Kwitega, washtakiwa wengine ni Ally Kibuga na Abdallah Mmanyi.

Hivyo, Kati ya mashtaka manne yanayowakabili washtakiwa hao, mashtaka matatu yanamkabili Kwitega peke yake.

Katika shtaka la kwanza, Kwitega Januari 24, 2022, katika hoteli ya Rumix iliyopo Kinondoni, kwa nia ya kutenda kosa, alimpa vidonge vya kumpumbaza mwanamke huyo, wakati akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Shtaka la pili, siku na eneo hilo, Kwitega anadaiwa kumbaka mwanamke huyo.

Shtaka la tatu, Kwitega alimuibia simu aina ya iPhone yenye thamani ya Sh3 milioni pamoja na nguo zenye thamani ya Sh300,000, vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Sh3.3milioni mali ya mwanamke huyo.

Shtaka la nne ni kupokea mali ya wizi tukio, linalowakabili mshtakiwa Kibuga na Mmanyi.

Kibuga na Mmanyi wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2022 walipokea simu aina ya iPhone yenye thamani ya Sh3 milioni, huku wakijua kuwa mali hiyo ni ya wizi.

Mbali na kesi hiyo, mshtakiwa Kwitega yeye anakabiliwa na kesi zingine nne ikiwemo ya unyang'anyi wa kutumia silaha mahakamani hapo na hivyo kukosa sifa ya kupata dhamana kwa kuwa shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha halina dhamana kwa mujibu wa sheria

Chanzo: mwanachidigital