Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kumteka mwanamke Dar wakosa dhamana

Hukumu Pc Data Wanaodaiwa kumteka mwanamke Dar wakosa dhamana

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Watu saba wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la unyang'anyi wa kutumia silaha na kumteka mwanamke mmoja aitwaye Han Hussein.

Washtakiwa hao ni Assad Abdulrasur (43) mkazi wa Msasaani Village; Farad Mussa (32) mkazi wa Airport Dodoma; Nathan Jothan (27) mkazi wa Sinza na Nicolas Nilahi (39) mkazi wa Wazo Hill.

Wengine ni Fredu Chahoza (49) mkazi wa Dodoma; Ifan Saleh (41) mkazi wa Kisemvule na Hassan Nur (39) mkazi wa Msasani Village A.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo, leo Oktoba 30, 2023 na kusomewa kesi ya Jinai namba 196/2023 na kusomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Neema Moshi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya.

Akiwasomea mashtaka yao, wakili Mosha amedai katika shtaka la kwanza ambalo ni unyang'anyi wa kutumia silaha, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Oktoba 16, 2023 katika eneo la Msasani Beach.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja waiiba simu aina ya iPhone yenye thamani ya Sh3.5 milioni; miwani moja ya macho yenye thamani ya Sh 300,000; pea moja hereni za dhahabu zenye thamani ya Sh 500,000; saa ya mkono yenye thamani ya dola za Marekani 120.

Vingine ni pochi moja ambayo ndani take ilikuwa na fedha taslimu Sh100,000, vyote vikiwa mali ya Han Nooh Hussein na kwamba washtakiwa hao walimtishia mlalamikaji huyo kwa bastola aina ya Glock 19, ili waweze kujipatia vitu hivyo bila kikwazo.

Shtaka la pili ni kuteka kwa nia ya kumdhibiti, ambapo washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Oktoba 16, 2023 eneo la Msasani Beach, lililopo wilaya Kinondoni.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa walitumia nguvu walimtaka Han Hussein aende Mtaa wa Ujirani uliopo Mbezi Beach na alipofika hapo, walimchukua na kumpeleka katika nyumba ya Haidary Waziri na kisha kumshikilia kwa siku nne mfululizo.

Washtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yao, walikana kutenda makosa hayo.

Upande wa mashtaka ilidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomewa hoja za awali.

Washtakiwa wakusudia kufanya majadiliano na DPP ya kuimaliza kesi:

Washtakiwa kupitia mawakili wao, Dismas Raphael na William Mkumbo, wameieleza Mahakama hiyo kuwa wanakusudia kufanya majadiliano na DPP ya kuimaliza kesi hiyo, wanaomba wateja wao wapangiwe tarehe fupi ili waweze kuretwa mahakamani.

"Kutokana na aina kesi inayowakabili wateja wetu, baada ya mahakama kupanga siku 14 kama Sheria inavyotaka, tunaomba iwapangie wateja wetu tarehe ya karibu ikiwezekani iwe Novemba 7, 2023 kwa sababu tunakusudia kufanya Plea Bargaing (kukiri mashtaka yao na kuomba kupunguziwa adhabu kwa njia majadiliano baina ya washtakiwa na DPP)," amesema wakili.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Moshi amewataka washtakiwa kufuata utaratibu kwa kuandika barua ya kukiri mashatka hao na kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) ili ipitiwe na kuangalia kama washtakiwa hao wanaweza kufanya majadiliano ya kuimaliza kesi hiyo.

Hakimu Lyamuya, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, aliwaambia washtakiwa hao, kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Baada ya hapo, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 7, 2023 itakapoitwa kwa ajili kutajwa na kuangalia kama washtakiwa wameweza kuandika barua kwenda kwa DPP.

Chanzo: mwanachidigital