Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kuiba silaha za IGP mstaafu wamwangukia DPP

Hukumu Pc Data Wanaodaiwa kuiba silaha za IGP mstaafu wamwangukia DPP

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Washtakiwa watatu kati ya wanne wanaodaiwa kuiba bunduki sita za aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, marehemu Harun Mahundi, wamemuandika barua Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) wakiomba kukiri mashtaka yao na kupunguziwa adhabu.

Washtakiwa hao, ambao watatu ni wafanyakazi wa ndani na mmoja ni mlinzi katika nyumba ya merehemu Mahundi, wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuiba na kumiliki silaha aina ya bstola na shortgun kinyume cha sharia.

Silaha hizo zina thamani ya Sh16milioni na ni mali ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, marehemu Harun Mahundi.

Waliomwandikia barua DPP kwa ajili ya kuimaliza kesi hiyo ni mfanyakazi wa ndani, Salum Mtani (20) na mkazi wa Mikocheni A; Zamba Likoti (43) mlinzi na mkazi wa Manzese Mburahati; Salum Zongo (45) mfanyakazi wa ndani na mkazi wa Manzese.

Hata hivyo, Hashim Omary, ambaye naye ni mfanyakazi wa ndani na mkazi wa Manzese, yeye hajamundikia DPP barua ya kukiri makosa yake.

Hayo yalielezwa jana Machi 2 na wakili wa Serikali Mosia Kaima mbele ya Hakimu Mkazi Kuu, Ramadhani Rugemarila, wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 71/2017 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Mosia alidai kuwa kutokana na washtakiwa hao watatu kuandika barua ya kukiri mashtaka yao, anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza vikao vya majadiliano na washtakiwa.

Hakimu Rugemarila baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 15, 2023 na washtakiwa Mtani, Likoti na Zongo, wapo rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana huku mshtakiwa Omary akiwa nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, wanashtakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 71/2027, ambapo wanadaiwa kutenda makosa yao katika maeneo matatu tofauti ikiwemo mkoani Morogoro.

Katika shtaka la kwanza, ambao ni la wizi wa silaha, washtakiwa wanadaiwa kati ya Mei na Septemba 2017 katika eneo la Mikocheni A, wilaya ya Kinondoni.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kuiba Bunduki sita, ambazo ni Rifle Remingon yenye namba B 6303058; Rifle H&H yenye namba 3085; Shortgun Winchester yenye namba 289112; Shortgun Pumb Action Winchestool yenye namba L. 1333952.

Silaha nyingine zinazodaiwa kuiba ni Pistol- Water yenye namba 320958 na Pistol Glock 19 yeye namba AYA 071, zote zikiwa na thamani ya Sh16, 240,000 mali ya hayati Harun Mahundi.

Shtaka la pili ni kumiliki silaha kinyume cha sheria ambapo bapo washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Oktoba 2, 2017 eneo la Mikocheni A, walikutwa wakimiliki silaha aina ya Rifle Remingon yenye namba B 6303058; Rifle H&H yenye namba 3085; Shortgun Winchester yenye namba 289112, bila kuwa na leseni kutoka kwa msajili wa sihala.

Shtaka la tatu ni kumiliki silaha kinyume cha sheria, ambapo washakiwa kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Septemba 28, 2017 eneo la Mikese mkoani Morogoro.

Siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa wakimiliki silaha aina ya Pistol Glock 19 yeye namba AYA 071 na Shortgun Pumb Action Winchestool yenye namb L. 1333952, bila kuwa na leseni kutoka kwa msajili wa sihala.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Novemba 8, 2017 hata hivyo kwa muda wote huo w miaka saba, upelelezi wa shauri hilo bdo haujakamilika.

Itakumbukwa kuwa Marehemu Mahundi ambaye alijiunga na jeshi la polisi mwaka 1960, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Desemba mosi 1984 hadi alipostafu Mei 3, 1996 na kabla ya kuwa IGP alishawahi kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, April 2, 2012 IGP Mahundi alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 72 na kuzimwa April 8, 2012 katika makaburi ya Kinondoni.

Chanzo: mwanachidigital