Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanane mbaroni kwa tuhuma za mauaji Kiteto

Kiteto Mhakamani Wanane mbaroni kwa tuhuma za mauaji Kiteto

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Watu watano wamesomewa shitaka la mauaji ya Amos Ephael (69) mkazi wa Kijiji cha Kazingumu, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara kwa tuhuma za mauaji.

Akisoma shitaka hilo Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Boniphace Lihamwike leo Agosti 14, 2023 amesema watuhumiwa hao kwa pamoja wametenda kosa hilo kinyume na kifo cha 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2022.

Hakimu Lihamwike amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Jastini Emmanuel (42) mkazi wa Kazingumu na mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Pima Peter (27) mkazi wa Langtomon,

Wengine ni Hamis Husein (24) mkazi wa Kibaya, Peter John (47) mkazi wa Langtimon na Neema Emmanue (27) mkazi wa Kazingumu.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walimpiga na kumsababishia kifo Amos Ephael (69) mkazi wa Kazingumu wakimtuhumu kuiba mahindi shambani.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Serikali, salimu Bakari amemweleza hakimu kuwa upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.

Katika tukio lingine watu watatu wa Kijiji cha Zambia, Kata ya Lengatei wilayani Kiteto wamesomewa shtaka la mauaji ya Issa Juma Bashiru (25) mkazi wa Kijiji cha Zambia.

Akisoma shtaka hilo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Mosi Soro Sasy Leo Agosti 14, 2023 amesema watuhumiwa hao wametenda kosa hilo kinyume cha kifo 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 kama iliyofanyiwa mapitio mwaka 2022.

Hakimu Sasy amewataja majina yao kuwa ni Muhina Athumani mtiti (37) mkazi wa Kijiji cha Zambia, Amni Kufinyu (26) mkazi wa Lengatei na Monjera Haji Shaban (25) mkazi wa Kijiji cha Zambia Kiteto.

Ilielezwa kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo la mauaji Agosti 5, 2023 kwa kumnyonga na kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni Issa Juma Bashiru usiku dukani kwake hapo kijijini.

Washtakiwa kwa pamoja hawakutakiwa kujibu chochote hivyo wamerejeshwa rumande hadi Agosti 28, 2023.

Chanzo: Mwananchi