Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanane mbaroni kwa kuiba vyuma vya nguzo za umeme

12116 Pic+tanesco TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Watu wanane wametiwa mbaroni na jeshi la polisi baada ya kubainika kufungua na kuiba vyuma vya Shirika la Umeme (Tanesco) katika nguzo za umeme wilayani Kilombero.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa ameyasema hayo leo Agosti 15 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana msako uliofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na Tanesco.

“Watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia vyuma hivyo katika matengenezo ya bidhaa mbalimbali ikiwamo mageti na kulisababishia shirika la umeme nchini hasara,” amesema.

Amesema wananchi wengi ambao si waadilifu wala waaminifu wamekuwa wakidiriki kukata na kuhujumu miundombinu ya Tanesco na wamekuwa wakiviuza vyuma hivyo kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo pia kutengeneza mitambo, majembe ya kulimia.

“Misako na operesheni hii itakuwa endelevu na kuibwa kwa vyumba kunaligharimu shirika fedha nyingi,”amesema kamanda Mutafungwa

Kwa upande wake ofisa usalama wa Tanesco mkoa wa Morogoro, Charles Ngwila amesema kuwa kumekuwa na vitendo vya hujuma dhidi ya miundombinu ya Tanesco ambapo vyuma vimekuwa vikiibiwa katika njia kuu za umeme.

Ngwila amesema katika operesheni hiyo vyuma 117 vimekamatwa katika wilaya ya Kilombero maeneo ya Mang’ula na Kibelege.

Chanzo: mwananchi.co.tz