Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanane mbaroni kutumikisha walemavu

Mbaroniiiiiiiii Wanane wakamatwa wakiwatumikisha wenye ulemavu

Fri, 11 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana nane kutoka katika mikoa ya Simiyu na Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuwatumia watu wenye ulemavu kama kitega uchumi cha kujipatia kipato.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha (DC), Saidi Mtanda amesema hayo leo Ijumaa Machi 11, 2022 wakati alipotembelea katika eneo la Ungalimited Mkoa wa Arusha huku akieleza kuwa kumekuwa na wimbi la kundi la watu kutoka katika maeneo mengine kuja na walemavu na kufanya biashara ya kuwatumikisha walemavu katika Mkoa wa Arusha.

"Tunalo kundi la vijana wengi kutoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Simiyu na Geita ambao wapo hapa Arusha wanawakusanya walemavu sio wa hapa Arusha na wanakaa chumba kimoja na yeye anakuwa anasukuma kiti cha mlemavu na yule mlemavu anaomba, usiku wanaweka kikao kwamba tumepata shilingi ngapi kwahiyo nasema kamanda wa polisi endelea na msako mkali " amesema DC Mtanda

Mmoja wa vijana waliokuwa wakifanya biashara hiyo haramu anayejulikana kwa jina la Mayenga, amedai kuwa anafanya hivyo kutokana na kuchanganywa na maisha.

Kijana huyo ambaye alitoka mkoani Simiyu amesema ana miezi miwili tangu aanze biashara hiyo.

"Mimi nimekuwa nikisukuma mlemavu kwenda katika eneo la tukio kuomba na tunatafutwa vijana kutoka sehemu nyingine kwaajili ya kuja kufanya kazi hii hapa mkoani Arusha baada ya kumaliza kuomba tunakwenda kuwachukua na tunagawana kiasi alichokipata kwa siku hiyo ambapo mimi mtu niliyekuwa namsukuma alikuwa akiingiza kwa siku Sh15,000  na tunagawana sawasawa na niliamua kufanya hivyo kutokana na maisha kunichanganya " amesema

Mtanda amewataka wananchi kuendelea kuimarisha amani na utulivu katika Wilaya hiyo kwa kufichua vitendo vya kihalifu katika maeneo yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live