Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa raia wa China walipa faini

97168 China+pic Wanandoa raia wa China walipa faini

Thu, 27 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ronglan Intl Industry and Trade Co. Ltd, Zheng Rongman (50) na mkewe Ou Ya (47) wamelipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kutoa rushwa ya Sh11.5 milioni kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Dk Edwin Mhede.

Wamelipa faini hiyo leo Jumatano Februari 26, 2020 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwakuta na hatia.

Kwa mara ya kwanza wanandoa hao raia wa China walifikishwa katika mahakama hiyo jana Jumanne Februari 25, 2020 kujibu shtaka hilo na kesi hiyo ilipangwa kuendelea leo kwa ajili ya kusomewa maelezo yao.

Mbali na kupigwa faini  mahakama hiyo imetaifisha Sh11.5milioni na kuwa mali ya Serikali.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakamani hiyo, Huruma Shaidi baada ya washtakiwa hao  kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa rushwa.

Rongman na Ya, ni raia wa China na wakazi wa Kinyambo, wilaya ya Mafinga mkoani Iringa.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz