Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa mbaroni kwa utapeli wa sh bil 14 kupitia sarafu ya kidigitali

Operanews1670062774951 Wanandoa mbaroni kwa utapeli wa sh bil 14 kupitia sarafu ya kidigitali

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Sri Lanka limeanzisha uchunguzi kuhusu udanganyifu mpya wa fedha ambao hadi sasa umehusisha utapeli wa Sh bilioni 14 huku watu 8,000 wakiwa waathirika katika mpango wa sarafu za kidijitali (cryptocurrency).

Msemaji wa polisi nchini humo, SSP Nihal Thalduwa amesema kuwa ulaghai huo unaodaiwa kufanywa na wanandoa wa China na raia wa Sri Lanka, umenza tangu 2020 ambapo watu 8,000 wametapeliwa.

Msemaji huyo amesema washukiwa hao walikuwa wakiwashawishi watu kuwa wakiwekeza katika sarafu ya crypto watapata faida kubwa.

Amesema wanandoa hao ndio waanzilishi wa ulaghai huo na walifanya wahanga hao kuwaamini kwa kuwaalika kwenye chakula cha heshima  cha jioni.

Uchunguzi huo unaofanywa na Idara ya Upepelezi ya Makosa ya Jinai (CID) ya Jeshi hilo imegundua kuwa matapeli hao waliwazuia wawekezaji waliowanasa kwenye mtego wao kutotoa faida zao walizopata kwenye uwekezaji huo.

“Wawekezaji hao walipojaribu kuondoa faida waliyopata kupitia uwekezaji huo, washukiwa hawakuwaruhusu kutoa fedha hizo” amesema SSP Thalduwa.

SSP Thalduwa amesema malalamiko kadhaa yamepokelewa katika kitengo cha Udanganyifu wa Kifedha cha CID.

“Baada ya uchunguzi wa muda mrefu, tuwakamata wenzi hao wa Kichina kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike walipojaribu kutoroka nchini. Wanandoa hao wa China kwa sasa wako rumande,” amesema na kuongeza kuwa;

Mshukiwa wa raia wa Sri lanka alikamatwa tarehe 11 Oktoba, 2022 na baadaye akaachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa kortini.

Jeshi hilo limekamata washukiwa wengine ambao wanaendelea kuwapeleleza juu ya tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live