Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa jela miaka mitano kwa kuwakeketa watoto wao

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro. Wanandoa wakazi wa Kijiji cha Kangala wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara nchini Tanzania wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya Sh600,000 baada ya kukutwa na hatia ya kuwakeketa watoto wao watatu.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, Lugano Kasebele ametoa hukumu hiyo jana Jumatatu Agosti 19,2019 katika mji mdogo wa Orkesumet baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao.

Amesema Thadey Parokwa (43) na Luwema Thadey (34) wametenda kosa hilo Machi 19, 2019 wakishirikiana na ngariba wa eneo hilo la Kangala.

"Mahakama imewatia hatiani mnahukumiwa kwenda jela  kwa kifungo cha miaka mitano au kulipa faini Sh600,000 ili iwe funzo kwa wengine," amesema Hakimu Kasebele.

Mahakama hiyo imewaamuru washtakiwa hao wawili kulipa Sh900,000 ya fidia ya kosa hilo.

Kutokana na kushindwa kulipa faini hiyo, walipelekwa rumande gerezani kutumikia kifungo hicho.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz