Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wakubali kumzika ndugu yao anayedaiwa kuuawa na polisi

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Hatimaye wananchi wameridhia kuzika mwili wa Jackson Charles baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Josephat Maganga kuwaomba kupokea mwili huo na kuahidi kuchukua hatua kali ndani ya siku mbili baada ya uchunguzi kufanyika.

Licha ya wananchi kuridhia kuzika leo Jumanne Machi 26, 2019 lakini mwili wa marehemu umeshindwa kuzikwa kutokana na familia hiyo kutokuwa na shamba.

Kutokana na hali hiyo mkuu wa wilaya aliagiza uongozi wa wilaya kutoa ardhi ili kijana huyo azikwe ambapo serikali ya kijiji imeridhia na kuahidi kutoa eneo lililopo Nyakafuro B kilomita tano kutoka katika eneo hilo.

Baada ya mwili kupelekwa katika nyumba aliyokuwa amepangisha vilio vilitawala baada ya watu kuona mazingira aliyokuwa akiishi.

Mkuu wa wilaya alishindwa kujizuia na kububujikwa machozi mara baada ya mwili kuingizwa ndani.

Maganga amesema hakuna mtu aliyeko juu ya sheria na endapo itathibitika sheria itachukua mkono wake.

Awali, baada ya wananchi kuridhia kuzika baba wa marehemu Charles Sengerema ameomba kusaidiwa Sh800,000 ili aweze kununua kiwanja atakachomzika mwanaye na kupata mahali pa kuishi jambo ambalo halikufanikiwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz