Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wachoma moto gari la afisa kilimo

Wananchi Wachoma Moto Gari La Afisa Kilimo Wananchi wachoma moto gari la afisa kilimo

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: millard

Wananchi wa Kijiji cha Kambai kilichopo Kata ya Kwezitu Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga wamechoma gari la Afisa Kilimo wa Kata jirani ya Tongwe aina ya Suzuki pamoja na kumjeruhi Afisa huyo wakimtuhumu kushindwa kusimamia maslahi ya Wananchi na kupelekea Wawekezaji kupewa eneo la zaidi ya ekari 500 bila tathmini ya kina kufanyika wala Wananchi kushirikishwa.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema baada tu ya kupokea taarifa hizo amelazimika kufika katika Kijiji hicho ili kufanya mkutano na Wananchi kwa lengo la kutafutia ufumbuzi suala hilo.

“Halmashauri ina eneo zaidi ya ekari elfu 3 lenye hati kwa zaidi ya miaka 28 lakini ndani ya kipindi cha miaka hiyo zaidi ya 28 hawajaliendeleza, alipatikana Mwekezaji wa kwanza mwaka 2020/2021 akapewa ekari 500 pasipo tathmini ya kina kufanyika kujua kiwango cha uvamizi kilichofanyika kwenye eneo hilo, mwaka jana 2023 wamepatikana Wawekezaji wengine wanne nao pia tathmini ya kina haikufanyika” DC Zainab ameiambia AyoTV.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Muheza (OCD), Hadija Sokolo amesema kwa sasa Afisa Kilimo huyo amelazwa Hospitali ya Wilaya Muheza akipatiwa matibabu na baadhi ya Watu waliohusika kuchoma gari hilo wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano.

Chanzo: millard