Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi waliovamia, kuharibu nyumba za walimu wachunguzwa

15299 Pic+wanafunzi TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imeunda tume ya kufuatilia na kuchunguza sababu ya baadhi ya wanafunzi wa shule ya wavulana ya Chidya kuvamia na kuharibu mali katika baadhi ya nyumba za walimu.

Shule hiyo inachukua wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi sita.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatatu, Septemba 3, 2018 mkuu wa wilaya ya hiyo, Selemani Mzee amesema usiku wa kuamkia jana baadhi ya wanafunzi walivamia nyumba ya mkuu wa shule, mwalimu wa taaluma na mwalimu wa malezi na kuharibu samani za ndani pamoja na kuchoma moto pikipiki mbili.

“Walivamia kwenye nyumba ya mwalimu wa taaluma, walivunja mlango wakaingia ndani wakaharibu samani za ndani, kwa mkuu wa shule hawakuharibu ndani waliharibu mita ya maji na mwalimu wa malezi waliingia ndani na kuharibu vitu vya ndani,”amesema Mzee.

“Walianzia kwa mwalimu wa taaluma na mkuu wa shule nyumba ziko jirani na walikuta pikipiki wakazichukua wakaenda kuzichoma moto, pikipiki moja ni ya mkuu wa shule na nyingine ni ya shule yenyewe ilinunuliwa mwaka jana.”

Mkuu huyo wa wilaya amesema, “kutoka hapo pana umbali kufika ilipo nyumba ya mwalimu wa malezi kwani unapita eneo la shule unaenda upande mwingine wa shule unakuta nyumba ya mwalimu wa malezi na nyumba za walimu wengine ambazo hazikuguswa.”

Amesema baada ya tukio hilo ulifanyika ukaguzi na kubainika baadhi ya wanafunzi hawapo shuleni na kwamba waliopo shuleni wanaendelea na masomo kama kawaida huku wenzao wa kidato cha nne wakijiandaa na mitihani.

“Usiku ule haikuwa rahisi kuwatambua lakini itakuwa ni mchanganyiko, hakuna mwanafunzi yeyote anayeshikiliwa kwa sababu walitoroka ndio sabababu nasema uchunguzi ukifanyika nitatoa majibu, kuna idadi ya wanafunzi hawapo,” amesema Mzee.

Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ameiomba serikali kutumia busara katika kushughulikia tukio hilo na kusikiliza pande zote na kupata muafaka na kukomesha matukio ya aina hiyo.

“Kilichofanywa na wanafunzi so kitendo kizuri lakini pia kufumbia macho madai yao si jambo jema, serikali itumie busara na kuwasikiliza wanafunzi, wao wana matatizo na walimu pia wana matatizo,” amesema Mwambe.

Chanzo: mwananchi.co.tz