Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanafunzi wa miaka 13 na 16 wadakwa wakiishi unyumba

63924 Pic+watoto

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Katika hali isiyo ya kawaida, Wanafunzi sita wenye umri kati ya miaka 13-16 wamekatwa baada ya watatu kati yao wa shule ya msingi, kutoroka nyumbani na kwenda kuishi unyumba na wanafunzi wa kiume wa Sekondari.

Wanafunzi wa kike ni wa darasa la saba katika Shule ya msingi Nyamalele wenye umri wa miaka 13 huku wa kiume wenye umri wa miaka 16 wakisoma Shule ya Sekondari Nkome.

Ofisa Mtendaji Kata ya Nkome, John Matanga ameliambia Mwananchi leo Jumapili Juni 23, 2019 kuwa watoto hao wamekamatwa usiku wa kuamkia jana Jumamosi Juni 22, 2019 saa saba baada ya kuwatafuta kwa siku tatu baada ya taarifa za wazazi kudai watoto wao wamepotea.

Matanga amesema wanafunzi hao walikamatwa kwenye nyumba ya Sophia Agustin ambaye mtoto wake wa kidato cha pili aliwakaribisha kuishi kwa siri katika chumba chake.

Matanga amesema wanafunzi hao walikutwa wakifanya mapenzi na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo ili iwe fundisho kwa wengine na kusema yanatokea hayo kutokana na  wazazi kutowajibika kwenye malezi.

Chanzo: mwananchi.co.tz