Makachero wa upelelezi wa jinai DCI wamewakatama wanafunzi wa chuo kikuu kwa madai ya kujihusisha katika visa vya uhalifu na ujambazi jijini Nairobi.
Kulingana na ripoti ya DCI, walimtia mbaroni kijana mmoja mweney umri wa miaka 19 ambaye ndio ameanza mwaka wake wa kwanza katika masomo ya chuo kikuu.
Visa vya wizi wa kimabavu vimekuwa vikikithiri katika mitaa ya Makadara, Kayole na Embakasi na kufuatia uchunguzi wa kinyemela, walimtia nguvuni kijana huyo wa chuo kikuu cha Kenyatta ambaye baadae aliwaelekeza kwa wenzake wengine watatu.
“Wakati wa oparesheni hiyo, Richard Lankisa, 18, Brian Kituku, 19 na Emmanuel Nyangwencha, 18, wote wakiwa wanasomea shahada ya Mafunzo ya Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta walikamatwa,” Sehemu ya ripoti hiyo ilisoma.
Baada ya msako wa kina uliofanyika katika chumba chao kimoja, ulipelekea kupatikana kwa bunduki aina ya glock, cartridges 8 maalum za 9×19mm, bastola tupu, barakoa moja ya plastiki nyeupe, vipakatalishi 2 vinavyosadikiwa kuwa ni mali ya wizi miongoni mwa vitu vingine.
Eneo la tukio lilishughulikiwa na maafisa wa upelelezi wa eneo la uhalifu katika DCI Thika na washukiwa hao walisindikizwa hadi kituo cha polisi cha Juja wakisubiri kuhojiwa zaidi na kufikishwa mahakamani.