Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamuua mwenzao kijijini wakimtuhumu kuzuia mvua

45165 Pic+auawa Wamuua mwenzao kijijini wakimtuhumu kuzuia mvua

Thu, 7 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkazi wa Mvumi Misheni wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Jonas Muhogo ameuawa na wananchi wa eneo hilo kwa imani za kishirikina akidaiwa kuzuia mvua isinyeshe.

Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde amesema leo Machi 6, 2019, kuwa mkazi huo aliuawa usiku wa kuamkia juzi kwa kupigwa mawe na marungu.

Amesema kuwa watu hao walivunja mlango wa nyumba yake na kumpiga kwa mawe na marungu huku mwanaye akifanikiwa kukimbia.

“Nasikitika sana kwa tukio lililojitokeza, niwaombe wananchi kutojichukulia hatua mkononi. Viongozi wa dini pia watusaidie kuomba ili tupate mvua za kutosha na jamii imrudie Mungu na kuacha imani za kiushirikina,” amesema Lusinde.

Amesema mkazi huyo ambaye kabla ya kifo chake alikuwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, alifia katika Hospitali ya Mvumi Misheni na kuzikwa jana kijijini hapo.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Venance Mgaiga amesema atalizungumzia suala hilo baada ya mwandishi wa habari hizi kufika hospitalini hapo.



Chanzo: mwananchi.co.tz