Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wambura afikishwa mahakamani Kisutu

41295 Pic+wambu Wambura afikishwa mahakamani Kisutu

Tue, 12 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Makamu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu akisubiria kupandishwa kizimbani.

Wambura amefikishwa mahakamani ikiwa ni muda mfupi baada ya kutoa taarifa kuamua kuachana na masuala ya mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa waandishi wa habari iliyotolewa na Wakili Emmanue Muga anayemsimamia kazi zake.

Katika taarifa hiyo, Wambura ameamua pia kuondoa kesi iliyokuwa mahakamani. Kesi hiyo alifungua kwa ajili ya kukazia hukumu ya Mahakama juu ya uamuzi wa kufungiwa kwake na TFF hapo awali.

Hata hivyo katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Wambura hajabainisha sababu hasa ya kuchukua uamuzi huo.

Taarifa za hivi karibuni zilidaiwa kuwa Wambura alishikiliwa na Takukuru kutoka na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha alipokuwa madarakani.



Chanzo: mwananchi.co.tz