Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wamalawi wawili wapandishwa kizimbani kwa kuishi nchini bila vibali

HUKUMU Wamalawi wawili wapandishwa kizimbani kwa kuishi nchini bila vibali

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa nne wa Malawi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kuingia na kuishi nchini kinyume na sheria

Washtakiwa hao Mika Banda, Teleza Zaile, Love Phiri, Innocent Nthali na Joseph Kheses walikutwa wakiishi nchini bila ya kuwa na nyaraka halali kutoka ofisi ya Uhamiaji.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali kutoka Uhamiaji Shijja, Sitta alidai mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Roda Ngimilango kuwa Septemba 12, 2023 eneo la Makongo juu Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Washtakiwa wote walikutwa wakiishi kinyume na sheria bila ya kuwa na nyaraka halali.

"Maeneo ya Makongo Juu, Wilaya ya Kinondoni washtakiwa wote wakiwa ni raia wa Malawi walikutwa wakiishi kinyume na sheria bila ya kuwa na nyaraka halali," alidai.

Hata hivyo, Sitta alidai baada ya kusomewa mashtaka yao washtakiwa wote walikiri kutenda makosa hayo na aliomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 27, 2023 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live