Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Walitaka kuniua" - Lengai Ole Sabaya

SABAYA3445 660x400 Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai , Lengai Ole Sabaya

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: MillardAyo

Aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameendelea kujitetea Mahakamani leo Arusha na kusema hajawahi kuwa na Msaidizi kwenye kazi zake lakini pia hawezi kuwataja Watu waliotaka kumuua.

Kuhusu tukio la kutaka kuuwawa alilolitaja Mahakamani hapo, Sabaya amesema akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alitishiwa kuuwawa na Watu hao wapo lakini hawezi kuwataja na kwamba taarifa za kutaka kuuwawa kwake zipo kwenye vyombo vya dola na zimeshafanyiwa kazi hivyo hawezi kuzielezea zaidi.

Kuhusu kushirikiana na Wasaidizi wake, Sabaya amesema hajawahi kuwa na Msaidizi yeyote kwenye kazi zake na kwamba Mshitakiwa wa pili ambae ni Sylvester Nyegu alimfahamu baada ya kupangiwa kazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai kufanya kazi kwenye ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Hai.

Chanzo: MillardAyo