Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliozamia Afrika Kusini walimwa faini Sh300,000

Nyundo Waliozamia Afrika Kusini walimwa faini Sh300,000

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Mwananchi

Watanzania 43 wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Kisutu kulipa faini ya Sh300, 000 kila mmoja au kwenda jela miezi mitatu kwa kosa la kwenda nchini Afrika Kusini bila ya kufuata taratibu za uhamiaji.

Akitoa hukumu hiyo leo Mei 8, 2023, Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Murio amesema baada ya washtakiwa hao kwa pamoja walikiri kosa lao hivyo mahakama imewatia hatiani.

Murio amesema mahakama imezingatia alichokisema wakili wa Serikali kuwa Serikali imeingia gharama kwa kuwasafirisha kurudi nchini pamoja na washtakiwa hao kuiomba mahakama iwapunguzie adhabu kali.

"Lengo la adhabu ni kumrekebisha mtu alichokifanya asirudie tena, wengi wenu mlioenda Afrika Kusini mliteseka hivyo mlitakiwa muombe kibali kwa kufuata taratibu na kanuni za nchi hizi na msirudie kosa muwe mabalozi kwa wenzenu," amesema Murio.

Awali, Wakili wa Serikali, Shija Sitta ameieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wapewe adhabu kali kwa kuwa Serikali imeingia gharama ya kuwasafirisha kurudi nchini.

Washtakiwa hao kwa pamoja waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu kali kwa kuwa walitumikia kifungo nchini Afrika Kusini.

Watuhumiwa hao kwa pamoja kwa tarehe isiyojulikana, waliondoka nchi bila ya kufuata taratibu za uhamiaji kuelekea Afrika Kusini.

Inadaiwa kuwa Mei 7, 2023 eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) washtakiwa hao walikutwa wameondoka nje ya Tanzania na kwenda kuishi nchini Afrika Kusini.

Chanzo: Mwananchi