Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliovamia nyumba  ya raia wa China wauawa

55133fba800a3297dc92f93620e8e207 Waliovamia nyumba  ya raia wa China wauawa

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika majibizano na polisi baada ya kuvamia nyumba ya meneja wa michezo ya kubahatisha raia wa China kwa nia ya kupora fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo alisema kuwa mkasa huo ulitokea Desemba 17, mwaka huu katika eneo la Kantalamba lililopo katika Manispaa ya Sumbawanga.

“Majambazi wawili wasiofamika kwa majina na makazi yao wanaokadiliwa kuwa na umri wa miaka 33 na 38 walifariki dunia wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa iliyopo katika Mji wa Sumbawanga baada ya kujeruhiwa kutokana na majibizano ya risasi kati yao na askari baada ya kuvamia nyumba ya meneja wa michezo ya kubahatisha raia wa China kwa nia ya kupora fedha,” alifafanua.

Alisema polisi walifika mapema eneo la tukio baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Aidha katika eneo la tukio imeokotwa bunduki moja inayotumia risasi za shotgun na maganda ya risasi pamoja na vifaa vya kuvunjia nondo na mikasi ya kukatia vyuma.

Chanzo: habarileo.co.tz