Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walioua kanisani wapandishwa kizimbani

Njombe Mahakama Jengo la Mahakama Wilayani Njombe

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe imetaja shauri namba 5 la mwaka 2022 linalowakabili Daniel Mwilango na Nikson Nyamideko wanaotuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Baraza la Walei Kanisa la Roman katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako, Dickson Myamba (48) ambaye aliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika duka lililopo ndani ya eneo la Kanisa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Matilda Kayombo amesema watuhumiwa Daniel Mwilango ambae ni Katekista (42) akishirikiana na Nikson Nyamwideko (23) wanadaiwa kuhusika na mauaji hayo February 7,2022.

Kesi imeahirishwa hadi February 28,2022 na Watuhumiwa wamerejeshwa rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.

Wawili hao wanadaiwa kumuua na kisha kumkatakata vipande Nickson Myamba katika Mtaa wa Mangula Mjini Makambako huku chanzo kikitajwa kuwa ni chuki binafs

Chanzo: www.tanzaniaweb.live